Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mwl. Vumilia Simbeye amewapa mkono wa heri walimu 10 wa michezo kutoka shule za msingi na sekondari wanaokwenda Mkoani Katavi kushiriki mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Akizungumza Ofisini kwake Mwl. Simbeye amewataka walimu hao kutumia vizuri muda wa mafunzo kuongeza ujuzi wa kuendeleza michezo shuleni.Aidha, Mwl. Simbeye amesema michezo ina mchango mkubwa katika kukuza nidhamu, afya na vipaji vya wanafunzi ili kuchochea maendeleo ya michezo katika Halmashauri ya Mji Kasulu. Kwa upande wake, Afisa Utamaduni wa Halmashauri hiyo Daudi Schinga amesema mafunzo hayo yatawasaidia walimu kuongeza uwezo wa kufundisha michezo.Baadhi ya walimu akiwemo Pastory Gahagi wa Shule ya Sekondari Hwazi na Epifania Mitima wa Shule ya Sekondari Mwilamvya Mpya wameishukuru Ofisi ya Mkurugenzi kwa kuwapa fursa hiyo wakiahidi kutumia vyema mafunzo hayo kuboresha michezo na kukuza vipaji vya wanafunzi.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254







Post a Comment