Kikao cha kawaida cha Kamati ya Lishe Wilaya kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha, kuanzia Januari hadi Machi, kimefanyika leo Mei 21, 2026 kwa lengo la kujadili hali ya lishe wilayani pamoja na tathmini ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za lishe katika kipindi hicho.Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ndugu Chiza Marando, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu ya lishe kwa wananchi ili kupunguza changamoto za utapiamlo na kuongeza uelewa kuhusu afya bora ya jamii.Mkurugenzi Marando ameagiza kuwa masuala ya lishe yawe ajenda ya kudumu katika vikao vyote vinavyofanywa na wataalamu wanapokwenda katika maeneo mbalimbali ya vijijini, ili kuhakikisha elimu ya lishe inawafikia wananchi moja kwa moja katika maeneo yao.Aidha, amesisitiza kuwa ushirikiano wa sekta mbalimbali unahitajika katika kuboresha hali ya lishe wilayani, huku akiwataka wataalamu kuendelea kutoa elimu ya matumizi bora ya vyakula vinavyopatikana katika mazingira ya wananchi kwa ajili ya kujenga jamii yenye afya na nguvu kazi bora.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment