Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tunduru (TUUWASA) inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha huduma ya maji safi mjini Tunduru kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maji yenye lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya uhakika na kuondoa changamoto ya upungufu wa maji katika maeneo mbalimbali ya mji huo.Hatua hiyo imejidhihirisha kupitia ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe.Denis Masanja, amefanya ukaguzi wa miradi mbalimbali muhimu ya maji inayotekelezwa ndani ya mji wa Tunduru ili kujionea maendeleo ya utekelezaji wake pamoja na kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.Katika ziara hiyo, Mhe. Masanja ametembelea maeneo ya ukarabati wa vyanzo vya maji vya Nanjoka Gravity na Mlingoti Gravity, ukarabati wa tenki la Frankweston pamoja na chanzo cha maji kilichopo kijiji cha Ngalinje. Aidha, alikagua ujenzi wa tenki jipya lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni moja za maji ambalo linatarajiwa kuhudumia vijiji 28 mara litakapokamilika.Kwa sasa, TUUWASA inatoa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira katika vijiji 32 pamoja na kata 8 ambazo ni Mchangani, Majengo, Nakayaya, Nanjoka, Mlingoti Mashariki, Mlingoti Magharibi, Masonya na Sisi kwa Sisi. Takwimu zinaonesha kuwa jumla ya wakazi 64,125 sawa na asilimia 78 ya wananchi wa maeneo hayo tayari wanapata huduma ya maji safi.Hata hivyo, kutokana na ongezeko la mahitaji ya maji kufuatia kukua kwa idadi ya watu pamoja na shughuli za kijamii na kiuchumi, kiwango cha maji kinachozalishwa kwa sasa hakitoshelezi mahitaji yaliyopo. Kutokana na hali hiyo, Serikali imeamua kuwekeza zaidi katika kuboresha miundombinu ya maji ili kuongeza uzalishaji na usambazaji wa huduma hiyo muhimu kwa wananchi.Katika utekelezaji wa mkakati huo, mnamo tarehe 07 Mei 2025, TUUWASA ilisaini mikataba mitatu yenye thamani ya shilingi bilioni 3,408,847,554.2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo ndani ya kipindi cha miezi 12.Vijiji vitakavyonufaika moja kwa moja na mradi huo ni Ujenzi, Kalonga, Extended, Lambai, Nakayaya Mashariki, Mchangani, Tulane, Ngalinje, Mkwanda, Majengo, Kalanje, Muungano, Nanjoka, NHC, Uwanja wa Ndege, Tanesco, Biasi na Kangomba.Mradi huo ukikamilika unatarajiwa kuongeza huduma ya maji safi kutoka asilimia 78 ya sasa hadi kufikia asilimia 100 kwa wananchi wa maeneo ya mjini Tunduru. Aidha, uzalishaji wa maji utaongezeka kutoka lita 3,704,024 hadi kufikia lita 8,283,224 kwa siku, hatua ambayo itaongeza upatikanaji wa maji safi na kupunguza changamoto iliyokuwa ikiwasumbua wananchi kwa muda mrefu.Utekelezaji wa miradi hiyo ni sehemu ya dhamira ya Serikali ya kuendelea kuboresha huduma za kijamii na kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu kwa maendeleo yao na ustawi wa jamii kwa ujumla.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254













Post a Comment