Na Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha.Maafisa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Shirika la umeme nchini TANESCO wameendelea kuonesha dhamira ya dhati ya kuleta mageuzi makubwa katika utoaji wa huduma za kidijitali kwa lengo la kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi.Akizungumza katika Kongamano hilo Mkurugenzi wa Mifumo ya Tehama nchini (ICT) wa Shirika la umeme nchini TANESCO David Bondo amesema kupitia matumizi ya mifumo ya kisasa ya kiteknolojia, shirika limeanza kuboresha huduma zake ili ziwe za haraka, rahisi na zenye uwazi mkubwa.Aidha ameongea kuwa hatua hiyo inaonyesha namna ambavyo taifa linaendelea kuendana na kasi ya mabadiliko ya kidijitali duniani.Amesema "Katika jitihada hizo, matumizi ya teknolojia yamekuwa nyenzo muhimu ya kurahisisha mawasiliano kati ya wananchi na watoa huduma. Huduma nyingi sasa zinaelekezwa kufanyika kwa njia ya kidijitali ili kupunguza usumbufu, kuongeza uwazi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa wakati" Hata hivyo maboresho hayo yanatajwa kuwa msingi muhimu wa kujenga taifa lenye matumizi makubwa ya teknolojia katika shughuli mbalimbali za maendeleo.Kwa upande wake Mratibu wa miradi wa maboresho Mifumo ya (TEHAMA) wa shirika la umeme nchini TANESCO Demitruce Dashina amesema katika sekta ya umeme, matumizi ya mita smart yameendelea kutajwa kuwa suluhisho muhimu litakalosaidia kuongeza usahihi wa matumizi ya umeme kwa wateja. Hata hivyo amesema kuwa Mita hizo zina uwezo wa kuonesha matumizi halisi ya umeme kwa wakati, jambo litakalomuwezesha mteja kufuatilia matumizi yake kwa urahisi na kupanga matumizi kwa uangalifu zaidi. Vile vile Mfumo huo pia unatarajiwa kuongeza uwajibikaji na kuondoa changamoto za makadirio yasiyo sahihi ya matumizi ya umeme. Teknolojia ya mita smart itasaidia kupunguza makosa ya usomaji wa mita pamoja na kudhibiti upotevu wa umeme unaoweza kujitokeza katika mifumo ya kawaida. "Kupitia mfumo huo wa kisasa, tutaongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha usalama wa taarifa za matumizi ya wateja, Hali hiyo itaongeza imani ya wananchi kwa huduma zinazotolewa na sekta ya umeme nchini.Wateja wataweza kupokea taarifa zao kupitia simu au mifumo ya mtandaoni, jambo litakalowasaidia kufahamu mwenendo wa matumizi yao kwa wakati.Mikakati hiyo inahusisha uwekezaji katika mifumo ya kidijitali, kuimarisha miundombinu ya TEHAMA pamoja na kutumia akili bandia na uchambuzi wa data katika kufanya maamuzi muhimu ya kiutendaji. Lengo kuu ni kuhakikisha huduma za umeme zinakuwa za uhakika, salama na zenye kukidhi mahitaji ya wananchi.Kongamano hilo limefunguliwa Kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO Lazaro Twange.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment