" USHINDI WA SIMBA SC DHIDI YA COASTAL UNION, WAONGEZA PRESHA KWA YANGA

USHINDI WA SIMBA SC DHIDI YA COASTAL UNION, WAONGEZA PRESHA KWA YANGA




Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo, Mei 21, 2026, katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mabao ya Simba SC yamefungwa na
Libase Gueye, Anicet Oura, huku bao la Coastal Union likifungwa na Maabad Maulid

Clatous Chama anaendelea kuonyesha ubora akitoa asisti mbili leo nakuwa mchezaji bora wa mechi (MOM) akiandika rekodi ya kubeba tuzo hizo mara tano mfululizo.

Kutokana na matokeo hayo, Simba SC imefikisha pointi 55 na kuendelea kushika nafasi ya kwanza ikiwa imecheza michezo 24. Wapinzani wao, Young Africans SC, wana pointi 54 wakiwa wamecheza michezo 23, huku wakishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Post a Comment

Previous Post Next Post