" WATOTO WAHIMIZWA KUWA WATIIFU

WATOTO WAHIMIZWA KUWA WATIIFU


Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha Katika maadhimisho ya siku  mtoto wa Afrika  na siku ya familia kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Ngarenaro Jijini Arusha watoto wamehimizwa kuwa watiifu, kusikiliza wazazi na kuepuka mnatumizi ya simu yanayopelekea kubadili mienendo yao ya utoto.Akihutubia mamia ya wananfunzi waliojumuika pamoja kusherehekea siku yao Afisa Tarafa ya Themi Chausiku Quam amesema wazazi watumie nafasi yao kukaa na watoto na kuwafundisha maadili hususan kipindi cha likizo.Aidha amesisitiza jamii kushirikiana na serikali  kuokoa na kutolea taarifa  watoto wanaoishi mazingira magumu na hatarishi ili kutengeneza taifa limara la kesho."Wazazi timizeni wajibu wenu Kwa kuwalea, kuwatunza na kuwapa haki zao za msingi ikiwemo kuwafundisha kazi za nyumbani, kuwasikiliza kwa upendo na watoto kufundishwa kutii na kuendana na maadili ya jamii zetu. Ikumbukwe mafanikio ya mtu yeyote yanaanza na msingi mzuri tangu akiwa mtoto" amesema Chausiku.Kwa upande wake Kaimu mkuu wa dawati la jinsia wilaya ya Arusha Hatibu Shaban amesisitiza wazazi na walezi kushirikiana na walimu Ili kujua  maendeleo yao,   kuwakagua watoto wao kila siku, na kutoa taarifa Kwa viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya mtaa pindi watoto wanapofanyiwa  vitendo vya ukatili.Sambamba na hayo amewataka watoto kujiepusha na vitendo vya matumizi ya dawa za kulevya kwani vinachangia kujiingiza katika vikundi hatarishi na  kukatiza ndoto zao.Katika namna hiyohiyo Afisa ustawi wa jamii Jiji la Arusha Nivo Kikaho amesema kuwa watoto wa mitaani wamezidi kuongezeka kutokana na sababu za kiuchumi ikiwemo umaskini pia migogoro ya kifamilia.Amesisitiza kuwa serikali Kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo itaendelea kuweka mikakati itakayosaidia kumaliza mianya inayochangia ongezeko la watoto wa mitaani.Vile vile Mwenyekiti wa mashirika yasiyo ya serikali Mkoani Arusha John Habibu amesema wataendelea kushirikiana na serikali Kwa lengo la kuona kila mtoto anapata uangalizi na kupata haki zake za msingi kama watoto wengine."Tutaendelea kuenzi maadhimisho haya kila mwaka kwa  kuhakikisha watoto wanapata haki zao za msingi kupendwa, kulindwa, kuheshimiwa, kusikilizwa na kupata uhuru wa kujieleza na nyingine nyingi"

 

Post a Comment

Previous Post Next Post