Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad, ametoa wito kwa wananchi hususan waendesha bodaboda kuendelea kulinda amani ya nchi, akisisitiza kuwa Watanzania hawana sehemu nyingine ya kukimbilia zaidi ya Mama Tanzania, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama, yenye umoja na utulivu.
Mhe. Azza ametoa wito huo leo Julai 18, 2026, wakati akizindua rasmi vituo vitatu vya waendesha bodaboda alivyovijenga katika Kata ya Tinde, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, ikiwa ni hatua ya kuwawezesha vijana kufanya shughuli zao katika mazingira rasmi na yenye utaratibu, huku akiwahimiza kufanya kazi kwa bidii na kutokubali kushawishiwa na yeyote kuvuruga amani.
Amesema amani ndiyo msingi wa maendeleo na kwamba bila utulivu shughuli za kiuchumi, ikiwemo usafirishaji wa abiria na mizigo, haziwezi kustawi, hivyo amewataka wananchi wa Itwangi kuwa mfano wa mshikamano, upendo, na utulivu.
Mbunge huyo amewataka vijana kutanguliza uzalendo na kutumia nguvu zao kujitafutia kipato halali badala ya kushawishiwa kufanya vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama, akisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inahitaji mazingira ya amani ili kunufaisha wananchi.
Mhe. Azza amewahimiza waendesha bodaboda kuwa mabalozi wa amani kwa kuelimishana, kuheshimu sheria, na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, akibainisha kuwa uzinduzi wa vituo hivyo ni sehemu ya juhudi zake za kuwawezesha vijana kufanya kazi katika mazingira salama na rasmi.
Mara baada ya uzinduzi huo, Mhe. Azza alikabidhi gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa Kituo cha Afya Tinde, gari lililotolewa na Serikali kwa lengo la kuimarisha huduma za afya, na baadaye viongozi wa mila wa Tinde walimtunuku zawadi ya vazi la kimila, fimbo ya heshima, na jina la kimila "Balele" lenye maana ya "Mlezi", kwa kutambua mchango wake katika kuwatumikia wananchi na kusimamia maendeleo jimboni humo.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment