Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Gloriana Kimath akipata maelezo mbalimbali kuhusu Maktaba hiyo kutoka kwa mwanzilishi wa From Hearts 2 Hands , Dkt. Briana Greene (kushoto) wakati wa uzinduzi rasmi wa maktaba wilayani Monduli.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Gloriana Kimath (kulia0 akipata maelezo mbalimbali kuhusu Maktaba hiyo kutoka kwa mwanzilishi wa From Hearts 2 Hands , Dkt. Briana Greene wakati wa uzinduzi rasmi wa maktaba wilayani Monduli.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli , Gloriana Kimath akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maktaba mpya iliyojegwa na Shirika la From Hearts 2 Hands kupitia mwanzilishi wake , Dkt. Briana Greene (kulia kwa Mkuu wa Wilaya) ambayo inafungua fursa ya kujifunza , utamaduni wa kujisomea , kupanua maarifa na kuongeza ufaulu wanafunzi wa Shule ya Msingi Lendikinya ya jamii ya wafugaji wa kimasai wilayani Monduli.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli , Gloriana Kimath akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maktaba mpya iliyojegwa na Shirika la From Hearts 2 Hands kupitia mwanzilishi wake , Dkt. Briana Greene (kulia kwa Mkuu wa Wilaya) ambayo inafungua fursa ya kujifunza , utamaduni wa kujisomea , kupanua maarifa na kuongeza ufaulu wanafunzi wa Shule ya Msingi Lendikinya ya jamii ya wafugaji wa kimasai wilayani Monduli.
Sehemu ya muonekano wa ndani wa maktaba hiyo ya kisasa
Sehemu ya muonekano wa ndani wa maktaba hiyo ya kisasa.
Sehemu ya muonekano wa nje wa maktaba hiyo ya kisasa.
***
SHIRIKA la From Hearts 2 Hands kupitia mwanzilishi wake , Dkt Briana Greene limezindua maktaba ya kisasa ambayo inaweza kuhudumia wanafunzi 737 wa Shule ya Msingi Lendikinya kutoka jamii ya wafugaji wa kimasai wilayani Monduli.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo , Mkuu wa Wilaya ya Monduli (DC), Gloriana Kimath ameipongeza taasisi hiyo kwa kujenga maktaba ambayo ni miongoni mwa maktaba bora zaidi katika Mkoa wa Arusha.
Amesema ushirikiano kati ya Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali umeendelea kuleta matokeo chanya katika kuboresha huduma za jamii, hususan sekta ya elimu hapa nchini.
"Ninatamani wakuu wa wilaya nyingine waje waione maktaba hii na wajifunze. Ni mradi wa mfano ambao umeongeza thamani kubwa katika elimu ya Wilaya ya Monduli," ameongeza.
Kimath amefafanua kwamba pamoja na uzuri wa jengo hilo, jambo muhimu zaidi ni kuhakikisha maktaba inatumika ipasavyo kwa kujenga utamaduni wa watoto kujisomea vitabu na kujifunza maarifa mapya.
Amesema ndani ya maktaba hiyo kuna vitabu vya historia, sayansi, lugha, sanaa na vifaa vya kujifunzia vitakavyowawezesha watoto kukuza vipaji na ubunifu wao.
Amewataka wazazi kuhakikisha watoto wanaendelea kujisomea hata wanaporejea nyumbani badala ya kuacha jukumu hilo kwa walimu pekee.
"Wazazi wana nafasi kubwa ya kuwajengea watoto utamaduni wa kusoma. Mtoto akitoka shuleni aendelee kupata muda wa kujisomea nyumbani," amefafanua.
Kimath amewahimiza wazazi wa jamii ya Kimasai kutowabagua watoto wa kike katika kupata elimu, akisema wao pia wana uwezo wa kufikia nafasi mbalimbali za uongozi.
"Mimi ni mtoto wa kike na leo nimekuwa Mkuu wa Wilaya wa kwanza mwanamke Monduli. Kama wazazi wangu wasingenisomesha, nisingefika hapa. Mtoto wa kike anaweza, tusimkatize ndoto zake kwa ukeketaji, ndoa za utotoni au vitendo vingine vinavyomnyima haki ya elimu," amesema.
Pia amewataka wananchi na viongozi wa kijiji kuilinda maktaba hiyo ili idumu kwa vizazi vijavyo, akisisitiza ni mali ya jamii nzima na si ya mtu mmoja ili kufanya vizuri kitaaluma.
Amewahimiza wakazi wa Monduli kuendelea kuwekeza katika elimu, akibainisha kuwa wilaya hiyo imeendelea kufanya vizuri kitaaluma.
"Elimu ndiyo ufunguo wa maisha. Katika matokeo ya Kidato cha Nne Mkoa wa Arusha, Monduli iliongoza, na katika matokeo ya Kidato cha Sita hatukuwa na Daraja la nne wala sifuri. Tukishirikiana Serikali, wazazi na walezi, tunaweza kufanya vizuri zaidi hadi ngazi ya taifa," amesema.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Dk. Briana Greene amesema uwekezaji katika elimu ni njia bora ya kubadilisha maisha ya watoto wa jamii ya wafugaji na kuwapa nafasi ya kufikia ndoto zao.
Ameongeza kwamba alianza kusaidia shule hiyo kwa kujenga tenki hilo la na miundombinu ya maji baada ya kubaini changamoto zilizokuwepo, kabla ya kuendelea na ujenzi wa maktaba kupitia taasisi yake ya From Hearts 2 Hands.
"Elimu ndiyo msingi wa maendeleo ya jamii yoyote,tunataka watoto wa Lendikinya wapate fursa sawa na watoto wengine duniani. Hii ndiyo sababu tuliamua kujenga maktaba yenye vitabu na vifaa vitakavyowasaidia kujifunza kwa njia mbalimbali," amesema.
Amesema maktaba hiyo imejengwa baada ya kuona umuhimu wa wanafunzi kupata vitabu karibu ili vifungue fursa ya kujifunza zaidi.
"Nakumbuka nilikuja Lendikinya na niliona watoto wakihitaji maji,tukatengeneza tenki la maji nikaona wanahitaji maktaba waweze kujisomea vitabu,nikaamua kuijenga hapa nashukuru kwa Serikali kwa ushirikiano wa kufanikisha hili".
"Natumaini utamaduni mzuri wa kimasai ikifanikiwa huku watoto wakipata fursa ya kupanua mawazo yao na kupata maarifa mapya yanayoweza kuleta maendeleo katika jamii yao ninafuraha kubwa kukutana nanyi na kuweza kutoa mchango wangu kwa jamii,"ameongeza.
Amewataka wazazi wa jamii ya Kimasai kuhakikisha wanawapeleka watoto wote shule, hususan wasichana, akisema elimu ndiyo njia ya kuvunja mzunguko wa umaskini na kuwawezesha watoto kujitegemea baadaye.
"Pia nawaomba wanafunzi kuitunza maktaba hii na vifaa vyote vilivyomo. Hii ni rasilimali yenu na itawasaidia kukua kielimu na kutimiza ndoto zenu," amesema.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi, diwani wa Kata ya Sepeko Joseph Kimaay, ameshukuru kwa ujenzi wa maktaba hiyo na kuwa itasaidia kukuza na kuboresha elimu.
"Katika kata na wilaya yetu kwa ujumla hakuna maktaba kama hui,tunashukuru kwa msaada huu na tunaamini bila ushirikiano mzuri wa Serikali na wadau binafsi leo tusingekuwa na jengo kama hili,tunaamini itaboresha elimu ya watoto wetu,"ameongeza.
Akisoma risala kabla ya uzinduzi huo, Mwalimu Mkuu Solomon. Godfrey amesema mradi huo ni wa kipekee katika Wilaya ya Monduli na unatarajiwa kubadilisha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wa shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1977.
Amesema shule hiyo ina wanafunzi 737, wakiwemo wavulana 331 na wasichana 406, pamoja na walimu wanane.
Godfrey ameongeza kuwa maktaba hiyo imewekewa samani, vitabu vya aina mbalimbali, vifaa vya michezo, muziki, sanaa, kompyuta na maeneo maalumu ya watoto kujifunzia kwa vitendo na kuwa uwepo wa maktaba hiyo utasaidia kuongeza utamaduni wa kujisomea kwa wanafunzi, walimu na jamii, kuchochea ubunifu, kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 86.02 kilichofikiwa mwaka 2025.
Mbali na maktaba hiyo, amesema shirika hilo limekuwa likitekeleza miradi mingine ya maendeleo katika kijiji hicho ikiwemo ujenzi wa tanki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita 100,000, ugawaji wa matenki ya maji kwa wananchi, ujenzi wa nyumba za kuvunia maji ya mvua na ugawaji wa chupa 700 za kubebea maji kwa wanafunzi.
Naye mwanafunzi wa Darasa la Sita, Riziki Papaking, amewashukuru wadau wa elimu kwa kufanikisha ujenzi wa maktaba hiyo, akisema itawawezesha kupata mazingira bora ya kujisomea na kuongeza ufaulu wao.
"Tunawashukuru wadau wa elimu kwa kutujengea maktaba hii. Itatupa nafasi ya kujisomea zaidi, kuongeza maarifa, kufanya vizuri katika masomo na kutimiza ndoto zetu," amesema Riziki.
Wanafunzi 737 wa Shule ya Msingi Lendikinya wilayani Monduli wanatarajiwa kunufaika na maktaba ya kisasa iliyojengwa na shirika la From Hearts 2 Hands, huku wadau wakisema mradi huo utakuza utamaduni wa kujisomea, kuongeza ufaulu na kuwapa watoto wa jamii ya wafugaji fursa sawa za elimu.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254











Post a Comment