Zaidi ya Sh milioni 35 za wakulima wa korosho ziko katika sintofahamu baada ya tani tisa za korosho kudaiwa kupotea katika Chama cha Msingi cha Ushirika Mwambesi, kilichopo Kata ya Misechela, Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, huku Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini, Mhandisi Fadhili Chilombe, akiagiza uchunguzi wa haraka na kuwawajibisha wote watakaobainika kuhusika.Tuhuma hizo ziliibuliwa katika mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama hicho, viongozi wa ushirika, Afisa Ushirika wa Wilaya, wawakilishi wa Chama Kikuu cha Ushirika (TAMCU) pamoja na Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini.Wanachama walidai kuwa tani tisa za korosho, sawa na kilo 9,000, zenye thamani inayokadiriwa kati ya Sh milioni 35 na 39 kwa bei ya msimu wa 2025/2026, zilipotea katika mazingira yasiyoeleweka, huku wakieleza kuwa fedha zilizotokana na mauzo yake hazikuingia kwenye akaunti ya chama wala kutolewa maelezo ya kuridhisha kuhusu matumizi yake.Aidha, wanachama hao walidai fedha za ushuru wa chama zilitumika kuwalipa baadhi ya wakulima bila idhini ya mkutano mkuu, jambo walilosema limeathiri shughuli za chama na kupunguza imani ya wanachama kwa viongozi wao.Akizungumza katika mkutano huo, Afisa Ushirika wa Wilaya ya Tunduru, Faodhi Motta, alisema ofisi yake ilifuata taratibu zote za kisheria kwa kufanya uchunguzi wa kina uliochukua zaidi ya mwezi mmoja na nusu kabla ya kuwasilisha taarifa kwa Mrajisi wa Vyama vya Ushirika ngazi ya mkoa kwa hatua zaidi.Hata hivyo, maelezo hayo hayakumridhisha Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini, Mhandisi Fadhili Chilombe, ambaye alihoji sababu za kucheleweshwa kwa hatua wakati suala hilo linahusu mali za wakulima zenye thamani ya mamilioni ya shilingi.Chilombe alisema viongozi wa ushirika wanapaswa kuwajibika kwa wakati na kuhakikisha maslahi ya wakulima yanalindwa, akisisitiza kuwa hakuna sababu ya ucheleweshaji katika kushughulikia tuhuma zinazohusu fedha na mazao ya wananchi.Alimtaka Afisa Ushirika kuhakikisha uchunguzi unakamilika kwa haraka, ukweli wote unawekwa wazi na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kuhusika na upotevu wa korosho hizo au matumizi yasiyo sahihi ya fedha za chama.Mbunge huyo alisema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mazingira ya kuongeza kipato cha wakulima kupitia ushirika, hivyo vitendo vya ubadhirifu au usimamizi usiozingatia sheria haviwezi kuvumiliwa kwa kuwa vinadhoofisha imani ya wakulima na juhudi za Serikali za kuboresha sekta ya kilimo.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment