" DEWJ NA DHAMIRA YA KUINUA MICHEZO KILWA KUSINI

DEWJ NA DHAMIRA YA KUINUA MICHEZO KILWA KUSINI

 



Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini, Mhe. Hasnain Gulamabbas Dewji, ameendelea kuonyesha dhamira yake ya kuendeleza sekta ya michezo kwa vitendo kupitia ugawaji wa vifaa mbalimbali vya michezo kwa vijana wa jimboni humo. Hatua hiyo inalenga kuhamasisha ushiriki wa vijana katika michezo na kuchochea maendeleo ya vipaji vyao.

Zoezi hilo safari hii limefanyika katika Kata ya Likawage, ambapo timu za vijana zimekabidhiwa seti za jezi pamoja na mipira kwa ajili ya kuimarisha shughuli za michezo. Vifaa hivyo vinatarajiwa kuongeza ari ya mazoezi na mashindano, sambamba na kuwapa vijana mazingira bora ya kukuza vipaji vyao.

Katika hafla hiyo ya ugawaji wa vifaa, Mhe. Dewji aliwakilishwa na Katibu wake, Ndugu Hamisi Kibarabara, ambaye aliwasilisha salamu za Mbunge kwa wananchi na vijana wa kata hiyo. Alisisitiza kuwa ofisi ya Mbunge itaendelea kushirikiana na makundi ya vijana katika kuendeleza michezo na shughuli nyingine za maendeleo.

Akizungumza kwa niaba ya Mhe. Dewji, Ndugu Kibarabara alisema kuwa michezo ni nyenzo muhimu ya kujenga afya, nidhamu, mshikamano na kuibua vipaji vinavyoweza kuwanufaisha vijana mmoja mmoja pamoja na taifa kwa ujumla. Aliongeza kuwa uwekezaji katika michezo ni uwekezaji wa moja kwa moja kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Kwa upande wao, vijana wa Kata ya Likawage walimshukuru Mhe. Hasnain Gulamabbas Dewji kwa msaada huo, wakieleza kuwa vifaa walivyopokea vitawawezesha kushiriki kikamilifu katika mashindano mbalimbali na kuendelea kukuza vipaji vyao.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254.

Post a Comment

Previous Post Next Post